FAHAMU SABABU YA YAMOTO BAND KUACHIA NYIMBO MFULULIZO 2014, JE UTARATIBU HUO UTAENDELEA 2015 AU LAA!

Bila shaka utakuwa ni shahidi kwamba Yamoto Band kwa mwaka 2014 walitoa nyimbo 5 na zote kwa karibu karibu sana bila kuziachia nafasi, lakini jambo zuri zaidi nyimbo zote zilizokuwa zikiachiwa na band hiyo zilionekana kuwa na mashiko kwa mashabiki mitaani, jambo ambalo ni nadra sana kufanywa na wasanii wengi wa muziki huo kwa kuhofia kuuzima wimbo unaokuwa umetangulia.

Hivyo basi kufuatia utaratibu huo Meneja wa bend hiyo, Said Fella amebainisha sababu zilizopelekea bendi hiyo kutoa nyimbo kwa mfululizo huo ambapo amesema kwamba moja ya sababu ni kutokana na vijana wa bend hiyo kukaa muda mrefu kipindi walipokuwa wakitengenezwa .


“Nimeanza kuwatengeneza wale tangu 2010, wengine nimewachukua 2011, kwahiyo ule muda wote waliokuwa wanakaa muda mwingi tukawa tunatengeneza ngoma zao. Kwahiyo ilivyoingia ile 2013 tulivyoanza kutoa ile moja mwezi wa nane ile Yamoto yenyewe, sasa nikaona mwaka unaokuja lazima tutoe nyimbo nyingi” alibainisha Fella


Fella aliendelea kusema kwamba Yamoto band hadi sasa ngoma zao zilizopo studio zinafika 19 na zote ni kali.


“Hawa madogo kwasababu pale studio ngoma zao zinafika hata 19 na zote ni kali” alisema Fella


Mbali na hayo Fella alisema lengo lingine la kuachia nyimbo nyingi mfululuzo ni kuhakikisha mashabiki wanapata furaha hususani katika show za bend hiyo.

Yamoto Band
Hata hivyo Fella aliendelea kusema kuwa licha ya kuwa kwasasa wameachia ngoma mpya ya ‘Ntakupwelepweta’ lakini anasema bado kuna ngoma kali zaidi ya hiyo ambayo wanatarajia kuizindua itakapofika mwezi wa 4 mwaka huu 2015.

Pamoja na hayo Fella alisema kuwa mpango walioutumia mwaka 2014 wakutoa nyimbo nyingi mfululizo hautaendelea kwani kwa mwaka huu 2015 wataachia nyimbo chache tu.


“Nimefikiria kwa mwaka huu sasa kwasababu tayari ngoma nyingi zipo kwa wateja wetu ..,mwaka huu nategemea Mungu akipenda nitoe zisizidi tatu”
alisema Fella


Wakati huo huo Fella amesema kwamba baada ya hivi karibuni Yamoto Band kufanya show, Kigali Rwanda show walioipata kupitia mwaliko wa Diamond Platnumz kwenye uwanja wa Amahoro uliokuwa umeajaa mashabiki 14,000, hatimaye sasa Yamoto band imepata mwaliko mwingine kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenda kufanya show U.K mwezi ujao.
 Endelea kuungana nasi kila siku kwa habari zaidi kutoka hapa habarimkusanyiko.blogspot.com, tafadhali mwambie na rafiki yako pia juu ya blog hii

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname