BEN POL: NILIWAHI KUVUTA BANGI KATIKA MAISHA YANGU


Staa wa mziki wa kizazi kipya anayefanya vizuri na ngoma yake ya Sophia kwa sasa Ben Pol amesema kuwa katika maisha yake aliwahi kuvuta bangi.
Akipiga story na Show ya Mkasi inayoruka kupitia EATV msanii huyo alikiri kuwahi kutumia bangi na kusema kuwa alifanya hivyo kipindi alipokuwa kidato cha sita.

“Pale kwenye maisha ya form five na six niliwahi kujaribu, sasa hivi situmii kilevi chochote, sivuti sinywi.” alisema Ben Pol.

Aidha, akielezea kuhusu safari yake ya mziki Ben Pol alisema alipokuwa kidato cha tatu washikaji zake walikuwa wakimwambia kuwa anaweza kuimba na sauti nzuri anayo pia, hivyo akajikuta akiigiza nyimbo za TID, Banana.

Msanii huyo alisema wakati akifanya yote hayo alikuwa anaupenda mziki, lakini hakuwa anajua ni nini anajitaji kwenye muziki.

“Nikawa napenda muziki lakini sijui exactly nataka nini kwenye muziki“ alisema

Hata hivyo anasema baadaye aliamua kwenda THT nakuanza mazoezi ya kuimba.

“Nikaenda THT, nikaambiwa imba nikaanza kuimba… nikatoa sauti wakasema lakini ana tone nzuri, nikapata zali nikaambiwa ingia darasani… Nikaanza na mimi kufundishwa, nikawa na-improve,” alisema Ben Pol.


Pamoja na hayo, msanii huyoanasema kabla hajatoka bado alikuwa na shahuku kubwa na kujiwekea nadhiri kuwa akipata naya kufanya na mtu ambaye yupo kwenye nafasi nzuri lazima akomeshee!

“Katika kitu ambacho kichwani kwangu nilikuwa natembea nacho nikasema nikikutana na mtu ambaye yupo kwenye nafasi nzuri akiniambia imba, namkomesha hatoki," alisema Ben Pol

Mbali na hayo Ben Pol pia hakusita kutaja orodha ya wasanii ambao huwa nafurahi anapokuwa nao, ambapo alimtaja Barnaba, Baba Levopamoja na AT.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname