HIKI NDICHO KINACHOFUATA BAADA YA FILAMU YA 'MZEE WA SWAGA'



Mkurugezi wa kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Jerusalem Films, Jacob Stephen ‘JB’ambae pia ni muigizaji na muongozaji wa filamu, ameswataka mashabiki wake kuwa tayari kwa kupokea mzigo mwingine baada ya wiki iliyopita kuiachia movie ya 'Mzee wa Swaga'
JB ambaye aliwashukuru wadau wake wa filamu kwa kuipokea vizuri filamu hiyo ya Mzee wa Swaga na kuwadokeza kuwa kwa sasa kampuni yake hiyo ipo katika mchakato wa kuachai movie nyingine itakayoitwa ‘Charle Mvuvi.’
Mbali na hayo, akielezea kuhusu movie hiyo, ambayo imewashirikisha mastaa kadhaa kama Hadji Adam, Shamsa Forda, Mzee Halikuni na Makombora, ambapo JB alisema movie hiyo imechezwa Zanzibar na inatarajiwa kutoka mwezi ujao.


Asante kwa kuendelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com unaweza tangaza nasi pia wasiliana nasi kwa simu namba 0656 268 623/ 0716 514 718 .

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname