FAHAMU ALICHOKISEMA DYANA NYANGE KUHUSU KUKUZA MZIKI WAKE




Mwanamziki wa kizazi kipya, Dyana Nyange amesema mwaka huu anamalengo ya kufanya collabo na wanamziki mahiri katika singo zake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwanadada huyo, ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja alisema katika nyimbo zake hizo zijazo atawashirikisha wakali wengine wa mzikikutoka Afrika Mashariki jambo litakalo leta ladha tofauti.
Msanii Dyana Nyange


Aidha, Dyana alisema malengo yake ni kuvuka mipaka ya Tanzania na kujikita kimataifa zaidi.

“Kwa mwaka huu nataka kuwashirikisha zaidi wanamziki nyota wa Afrika Mashariki”, alisema Dyana huku akiongeza kuwa lengo lake ni kukonga nyoyo za mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname