UPENDO KILAHIRO APANIA TAMASHA LA PASAKA



Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Upendo Kilahiro amesema ikiwa atapata fursa ya kushiriki katika miaka 15 ya Tamasha la Pasaka mwaka huu, atahakikisha anaimba nyimbo zilizopo katika albamu yake mpya inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.


Kwa mujibu wa mwimbaji huyo anasema tamasha hilo ni maalum sana kwa sababu linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, hivyo akipata nafasi ataimba nyimbo mpya na kuwa kama zawadi kwa Watanzania.

Hata hivyo, Kilahiro hakuataka kutaja nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo mpya akidai kuwa bado ni mapema na lengo lake ni kuwashitukiza Watanzania watakaopata nafasi ya kuhudhulia tamasha hilo.

Pamoja na hayo, Kilahiro alisema licha ya kuhitaji kuimba nyimbo hizo mpya, lakini pia anaimba na zile za zamani ambazo zinatamba katika Nyanja ya nyimbo za injili na kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.

Tamasha hilo la Pasaka linatarajiwa kufanyika Aprili 5 mwaka huu.

Shukrani kwa kuendelea kuwa karibu nasi katika kupashana habari msomaji wetu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname