TID AKANA KUTOMDHULUMU Q- CHIEF KUHUSU PESA ZA TOP BAND BALI ILIKUWA NI TAMAA TU


Staa wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama ‘Mnyama’ hapa namzungumzia TID amesema kuwa tamaa ndio kitu kilicho sababisha kumuondoa Q- Chief kwenye kundi lililokuwa linaitwa Top Band.

Hayo yameibuka kupitia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, ambapo msanii Q- Chief alisema sababu za yeye kujiondoa Top Band ni baada ya TID kumdhulumu kiasi cha mamilioni ya shilingi yaliyotokana na albamu ya bendi hiyo.

Pamoja na madai hayo ya Q-Chief , lakini TID naye kupitia kipindi hicho hicho alikanusha madai hayo na kusema kuwa hiyo haikuwa sababu ya yote hayo bali Q-Chief alikuwa na tamaa.

TID katika kulielezea hilo alisema kuwa kimsingi fedha hizo zilikuwa zake kwa kuwa yeye ndiye aliyeandika nyimbo za albamu hiyo na kutoa jina na zaidi yeye ndiye aliyefikia hata makubaliano na mhindi juu ya kuiuza albamu hiyo.

Hata hivyo, TID aliendelea kusema kuwa baada ya kulipwa fedha hizo walikuwa wamekubaliana kuwa zingetumika kununua vyombo kwa ajili ya bendi, huku akisema pia Q-Chief alipewa fedha kadhaa ambazo aliishia kuzitumia vibaya na zilipokwisha aliamua kuchukua polisi na kumwendea na kudai kuwa alimdhulumu.
Shukrani za pekee kwako msomaji wetu kwa kuendelea kuwa nasi.



No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname