JE, HII KAULI YA MSANII HUYU INAWEZA KUSABABISHA SOKO LA BONGO MOVIE KUTOFIKA KIMATAIFA?


Muigizaji mkongwe na muongozaji wa filamu hapa Bongo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Jerusalem, Jacob stephen 'JB' amesema umri wake umeenda hivyo itamuwia vigumu kuifikisha tasnia hiyo kimataifa.
Hayo aliyasema wakati akijibu baadhi ya maswali ya mashabiki wake ambao walitaka kumuona msanii huyo akifanya kazi na wasanii wa kimataifa ili kufanya tasnia hiyo kutanuka zaidi.

Akijibu maswali ya mashabiki hao JB alisema “ndugu zangu kwanza nashukuru kwa kuniona nafaa kuwawakilisha kimataifa, lakini mwenzenu umri umekwenda.kitaalamu umri mzuri wa kuanza utafutaji ni 20-35.nina zaidi ya 40.nguvu zimepungua ndio maana akili yangu naiweka zaidi kuwa producer kupitia Jerusalem zaidi kuliko kuigiza” alisema.

Muigizaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Jerusalem, Jacob Stephen 'JB
Mbali na hayo JB alisema ndoto zake ni kuifanya kampuni yake kuwa kubwa Afrika ili waigizaji wa nje watamani kufanya kazi naye.

Lengo ni filamu yetu moja kuja kuuzwa zaidi ya billion 1 na inawezekana kwa sababu soko lipo na mchakato umeshaanza subirini soko halitafutwi linajengwa, tuamke, tusifikiri kikawaida tufikiri tofauti In Jesus Name. ..” JB alisisitiza hivyo na kumaliza.
Asanteni wasomaji wetu kwa kuendelea kufuatilia habari kupitia sisi, tunatambia sana uwepo wenu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname