FAHAMU SABABU ZA BAADHI YA WANAUME KUSHINDWA KUFIKA KILELENI

Mwanaume kushindwa kufika kileleni ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua wanaume na linapotokea wenge huumia sana na hata kuathirika kisaikolojia.
Tatizo hili la mwanaume kushindwa kufika kileleni, hii ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa utoaji wa manii wakati anashiriki tendo la ndoa. Tatizo humfanya mwanaume kutofurahia tendo hilo na hata kuchangia kuharibika kwa mahusiano.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa kitaalam tatizo hili huchangiwa na ‘hyponadism’ hii ni ile hali ya korodani kushindwa kuzalisha kichocheo (hormone) aina ya ‘testosterone’ kwa wingi. Hivyo hali hiyo huweza kusababisha kutozalishwa kwa mbegu za kiume na kupungua kwa hisia wakati wa tendo la ndoa na wakati wa utoaji wa manii.

Pia sababu nyingine ni suala la magonjwa yanayoathiri tezi dume, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na ‘prostate cancer’ ‘prostatisis,’ n.k. magonjwa hayo kwa ujumla wake huweza kuwa chanzo cha tatizo hilo kwani hupunguza uwezo wa usafirishaji wa mawasiliano kati ya ubongo na viungo vya uzazi.

Mtaalam huyo anaendelea kueleza sababu nyingine za tatizo hilo kuwa ni pamoja na mazingira ya kushiriki tendo, hii ni maana ya utulivu na hata usafi wa maeneo ya faragha. Hivyo, mazingira yasipokuwa yenye kumridhisha kila mmoja katika tendo hilo huweza kupelekea mwanaume asifike kileleni.

Ajali pia ni chanzo kingine cha tatizo hili, hii huwa mbaya zaidi endapo mhusika atakuwa ameumia kwenye viungo vya uzazi hususani korodani, uume au tezi dume n.k

Mbali na sababu hizo, Dk Mandai anasema, uchovu wa mwili pia ni chanzo kingine kinachoweza kupelekea mwanaume kukosa msisimko wa kutosha, hivyo kupelekea utokaji wa manii ukawa wa shida au kama atatoa anaweza asipate taarifa kama ametoa manii hayo.

Magonjwa yanayoharibu mfumo wa fahamu, ni chanzo kingine cha tatizo la wanaume kushindwa kufika kileleni, magonjwa hayo ni kama kisukari, kiharusi pamoja na shinikizo la damu.

Sababu zipo nyingi mpendwa msomaji wetu, lakini hizo ni baadhi tu zinazoweza kuchangia tatizo hilo, lakini endapo unapenda muendelezo wa mada hii ingia www.dkmandai.com utapata muendelezo wa mada hii yote.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname