FAHAMU HAYA MACHACHE KUHUSU SANAMU LA ASKARI LILIPO KATIKA YA JIJI LA DAR ES SALAAM


Jiji la Dar es salaam ni mmoja ya majiji yenye vivutio vya kitalii vipatikanavyo katika viunga tofauti tofauti katika jiji hili. Moja ya kivutio cha kitali ni Sanamu la Askari.
Sanamu la askari hii ni kumbukumbu ya askari ambao walipigana kwenye Jeshi la Waingereza katika vita ya kwanza ya dunia. Ikiwa sanamu ili limesimama katika ya mzunguko kati ya barabara ya Samora na Maktaba sehemu ambayo pia inasemekana ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam. Sanamu hilo la askari liliwekwa mnamo mwaka 1927.

Kitambulisho kikubwa cha sanamu ili ni anaonekana askari ambaye amevalia sale za jeshi la mkoloni uku akiwa ameshika gobore lenye kisu mbele yake. Sanamu ili lilitengenezwa nchini Uingereza na James Alexander Stevenson kabla ya kusafirishwa na kuletwa Dar es Salaam.
Sehemu ambayo leo hii inaoneka sanamu la askari hapo awali katika ukoloni wa Mjerumani kulikuwa na sanamu la gavana wao ambeye ni Hermann Von Wissmann ambalo liliwekwa mwaka 1911, likaweza kutolewa na Waingereza mwaka 1916 baada ya wao kuwasili Dar es Salaam.

Hizo ndizo details fupi kuhusu sanamu la Askari linaptikana katika ya jiji la Dar es Salaam.

Mambo yote hayo yanayohusu masuala ya utalii huandaliwa na Shadrack D. Daniel kutoka kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's Ltd, ambao ni mabingwa wa kuandaa safari za kitalii pamoja na kukodisha magari kwa gharama nafuu sana, endapo ungependa kujaribu huduma zao hebu watafute kwa simu namba 0654 022 054 / 0715 437 283 au kupitia www.samscarental.com.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname