KINGWENDU ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU


Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa nchini, Rashid Mwinshehe maarufu kama "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge mwaka huu 2015.
Hata hivyo, Kingwendu hakuweka bayana atagombea jimbo gani wala kupitia chama gani, isipokuwa zaidi alisema kuwa chama ambacho kinapendwa na Watanzania wengi ndicho atatumia tiketi yake.

Akizungumza na mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema, "Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi kwenye jimbo ambalo nitalitaja hapo baadae wakati utakapofika, Bado ninafanya mazungumzo na washauri wangu wa karibu kuhusiana na swala hili, nadhani nitaliweka wazi muda ukifika..." Zaidi nawatakia Watanzania kila la kheri katika harakati hizi".
Msanii wa vichekesho Kingwendu.
 Kufuatia kauli hiyo wataalamu wa masuala ya kisiasa nchini, wameitafsiri kauli hiyo ya kingwendu kwa mitazamo tofauti, huku wengi kati yao wakisema kuwa upinzani una nguvu kubwa hivi sasa hapa nchini, hivyo sio ajabu kwamba yawezekana msanii huyu amevutiwa na kuamua kujiunga na chama fulani cha upinzani ili aendeshe harakati za ukombozi wa taifa hili.


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname