HII NDIYO AINA YA MALORI MAPYA YENYE TV NYUMA AMBAYO HUMSAIDIA DEREVA ANAYEKUJA NYUMA KUONA KILA KITU MBELE HASA WAKATI WA KU-OVERTAKE


Leo nimepata bahati ya kuifahamu hii teknolojia mpya ya haya malori yenye TV nyuma ambayo huweza kumuonesha dereva wa gari linalokuja nyuma kila kitu kinachoendelea mbele na hivyo kumrahisishia dereva wa nyuma ku-overtake kwa urahisi na kuepuka ajali.

Ni ukweli usiopingika kuwa ishu ya ajali za barabarani imekuwa ni tatizo kubwa katika nchi mbalimbali duniani hasa nchi zetu hizi zinazoendelea.

 Kampuni ya Samsung imeamua kuja na haya malori ambayo yamefungwa 'screen' nyuma ambayo humuonesha dereva atakayekuwa nyuma ya lori hilo kila kitu kinachoendelea mbele na hivyo kumrahisishia hata ku- overtake kwa sababu atakuwa anaona vizuri kilichopo mbele.

Teknolojia hiyo inahusisha utumiaji wa kamera maalum ambazo zimefungwa mbele ya lori na kuonesha TV kubwa inayokuwa sehemu ya nyuma ya lori.

Wanasansi na wataalam wanasema kuwa TV hiyo imetengenezwa kwa vioo maalum na hivyo kuifanya iwe imara na kutovunjika kwa urahisi.

 Aidha, imeelezwa kuwa  TV zilizofungwa nyuma ya malori hayo zinauwezo wa kuonekana vizuri hata nyakati za usiku pia.

Samsung wanasema teknolojia hiyo itasaidia kuzuia ajali za aina mbalimbali za barabarani ikiwa zile zinazosababishwa na maamuzi ya wakati wa ku-overtake au ajali zinazotokana na malori kufunga break za ghafla kutokana na wanyama au watu kuvuka barabara ghafla.

Kufikia hivi sasa magari hayo tayari yamefanyiwa majaribio nchini Argentina ambayo ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ajali za malori na hadi sasa wengi wameisifu sana teknolojia hiyo.

 Hapa kuna video ya jinsi gari hiyo inavyoonekana ikiwa barabarani>>

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname