PROF: LIPUMBA AJIUZULU NAFASI YA UENYEKITI CUF

Jana zilikuwa kama stori tu hivi amabazo hazikuwa na uhakika sana kuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho, lakini leo Lipumba katangaza mwenyewe mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa amejiuzulu.

Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.

Aidha, Lipumba amesema UKAWA ilianzishwa ili kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.

Mbali na hayo Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname