TFDA YAANIKA RIPOTI KUHUSU THAMANI NA IDADI YA VIPODOZI VYOTE VILIVYOTEKETEZWA 2014/ 2015

 
Kuna baadhi ya vipodozi ambavyo vimekuwa vikipigwa vita na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kutokana na vipidozi hivyo kuwa na madhara kwa watumiaji.

Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA imetoa ripoti ya mwaka wa fedha kuhusu bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria na hatua zilizochukuliwa.

Akitoa ripoti hiyo Mkurugenzi wa TFDA Hitti Sillo amesema katika mwaka wa fedha wamekamata na kuteketeza vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku tani 16.61 ambazo thamani yake ni shilingi milioni 44.2.

‘Vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku vilivyoingizwa tumekamata vikiwa vinaingizwa nchini na vingine vimekutwa katika soko vikiwa tayari vimeingizwa na vingine vikiwa njiani kuingizwa nchini, mara nyingine tumekamata mabasi yakiwa na vipodozi vinavyoingizwa nchini kinyume cha sheria vyote hivyo thamani yake kwa mwaka wa fedha uliopita ni shilingi milioni 44″ Sillo.

Hata hivyo Sillo amesema kazi hiyo ni endelevu kwa kuwa TFDA ipo sehemu mbalimbali nchini na wakaguzi wake wapo kuanzia bandarini na katika viwanja vya ndege ambapo ndipo hukamataa bidhaa nyingi.

Mbali na hayo,Sillo amesema miaka mitatu iliyopita udhibiti umeimarika sana ndio maana matukio mengi ya kukamatwa kwa watu ambao wanaingiza vipodozi hatari kinyume cha sheria wanakamatwa wakiwa mipakani.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname