RAIS MAGUFULI KAMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE HOSPITALINI


Kumekuwa na ripoti mfululizo kwenye vyombo vya habari kuhusu kuumwa na kulazwa kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye katika hospitali ya Muhimbili huku kukiwa hakuna ripoti inayotaarifu ugonjwa wake.



Rais Magufuli kaamua kufika katika Hospitali ya Muhimbili na kwenda kumjulia hali mzee Sumaye japokuwa hata yeye mwenyewe hakuwa na taarifa ya ujio wa ugeni wa Rais.


AM POMBE
Akizungumza baada ya kuonana na Rais Magufuli Mh Sumaye amesema "Nimeshukuru sana Rais kuja kunitembelea hapa ni jambo kubwa, nimeshtuka kwa sababu sikutegemeana sikupata taarifa yoyote…. namshukuru Rais Magufuli kwa upendo wake, anaonesha kujali sana watu wake" alisema Frederick Sumaye.

Katika hatua nyingine Mh. Sumaye amesema "Naendelea vizuri, hali yangu ni nzuri natumaini baada ya muda mfupi nitatoka hospitali" Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Source: Millard ayo.com


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname