SAMMATA AENDELEA KUPOKEA PONGEZI ZAKE AWAMU HII NI KUTOKA KWA JK


Baada ya Mbwana Samatta kufanikiwa kushinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe Jakaya Mrisho Kikwete naye ameonana na mchezaji huyo na kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na mchezaji huyo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo pia Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye alihudhuria.

PICHA ZOTE NA BASHIRI NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname