WASTARA KAYASEMA HAYA BAADA YA KUFANIKIWA KUFUNGA NDOA NA MBUNGE



WASTARA X
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi zilizokuwa zikimuhusu muigizaji Wastara kufunga ndoa na mtu aliyetajwa kuwa ni Mbunge.

Hatimaye tetesi hizo zimekata baada ya kubainika kuwa ni kweli muigizaji huyo kafunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge Zanzibar, Sadifa Khamis Juma. ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM).


WASTARA VIII
Wastara kapost picha kwenye account ya Instagram na kuandika haya >>’Nilikuwa kwenye usingizi mzito nimeshtuka nikakumbuka ni vizuri kuwapa asante wale wote walipiga goti kuniombea siku moja nipate faraja au tulizo la moyo ama stara kwa mwanamke wa kiislam kama dini inavyosema.. Japo kwangu nilikuwa nimeweka nadhiri ya miaka 3 ikipita basi ridhki ya mume ikija milango iko wazi alhamdulilah imekuja wakati muafaka na siku muafaka baada nadhiri yangu kutimia. Mungu ni mwema sana namuamini sana na ananipenda sana ndio maana kaniumba anavyojua yeye tumshukuru mungu kwa hili, najiombea na wale wenye nia njema na mim tuwe pamoja, iwe yenye neema ndoa hii aliyoipanga mungu pekee yeye ndie mwenye mamlaka juu ya hili barka, rehma, stara, uvumilivu ridhiki, upendo uwe juu yetu na bi mkubwa niliyemkuta aliyenipokea kwa mikono miwili kma mke mwenziwe msiumize vichwa tunajuana tunaheshimiana.’- @wastara84

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname