WANANCHI WAASWA KUCHAGUA VIONGOZI WAPENDA MAENDELEO


Mwanza, Na Goodluck Ngowi
Wananchi wametakiwa kujenga tabia ya kuchagua viongozi walio na sifa ambao wanapenda maendeleo ya wananchi bila kujali maslahi yao binafsi kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi hivi sasa.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwishoni mwa wiki iliyopita  katika uwanja wa Mahina kati, ambapo Diwani wa kata ya Mahina, Charles Chinchibela aliwasihi wananchi kuepukana na wanasiasa wa kwenye kahawa.

“Epukaneni na wanasiasa wanaozungumza siasa za kwenye kahawa, ambapo kila mtu anajifanya mjuaji kumbe hajui  sikilizeni siasa za maendeleo ambazo zitawasaidia ndani ya miaka mitano”. Alisema Chinchibela

Mbali na hayo, diwani huyo alisema kuwa, wananchi wanapaswa kuwa makini na viongozi wadanganyifu wanaodai kuwa yeye hajafanya kitu, huku wakijua kuwa uchaguzi huu mdogo ndio taswira ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Naye, mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti katika eneo hilo la Mahina kati Pascal Bulabo aliwataka wananchi hao kumpigia kura siku ikifika ili kuleta maendeleo yaliyoshindwa kuletwa na chama tawala.

“CCM wameshindwa kwa miaka yote hiyo kuleta maendeleo, imefika wakati kwa wakazi wa Mahina kuchagua CHADEMA, kwa kuwa ni chama kinachopenda maendeleo kwa watu wake”. Alisema Bulabo.

Endelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com kwa kupata habari zaidi, nasi tunaahidi kuwa nawe kila iitwapo leo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname