WATANZANIA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI BORA



 Arusha, Na Theo M George.

Watanzania wametakiwa kuwa makini na viongozi wanao wachagua kuongoza wananchi kwa kuangalia vigezo vya utendaji kazi kwa maslahi ya wananchi na sio ushabiki wa kivyama.

Hayo yamesemwa jana na Diwani wa kata ya Elerai Jeremiah Mpinga wakati wa kumnadi mgombea Jonas Bethuel Temba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) katika kampeni zinazo endelea jijini Arusha za kuwachagua wenyekiti wa mitaa.

Mpinga aliesema kuwa, wananchi wanapaswa kutambua kuwa kiongozi bora ni yule anayejali na kutetea haki za wanyonge na taifa kwa ujumla kwa kuboresha miundo mbinu na kwa kuzingatia huduma bora za kijamii ikiwemo huduma za afya, kiuchumi na kufuata demokrasia iliyo na maslahi kwa taifa na sio kwa manufaa ya chama.

Aidha, aliongeza kuwa, taifa linahitaji viongozi waadilifu na kusisitiza kuwa endapo mgombea atachaguliwa na wananchi na atashindwa kutekeleza aliyo yaahidi wakati wa kampeni zake uongozi na wananchi watachukua jukumu la kumuondoa madarakani kama ilivyofanyika kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho  katika mitaa mbalimali ambao walichaguliwa kupitia chama hicho.

Naye mgombea Jonasi Bethuel Temba, amewasisitiza wananchi kumpigia kura na kuwataka wajitokeze kwa wingi  mara ifikapo Desemba 14, 2014, ili taifa liweze kupata viongozi bora watakao liongoza taifa kwa misingi ya kidemokrasia na maslahi ya taifa kwa ujumla.




Unastahili kupata taarifa zote kutoka hapa nchini kupita habarimkusanyiko.blogspot.com, asante kwa kuendelea kutuunga mkono

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname