
Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho Januari 17 saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili na endapo kituo chochote kitakaidi basi kitachukuliwa hatua kali za sheria.